Thursday, March 27, 2014

OSTAZ JUMA AKAZIA UCHUMBA KWA JOHARI

Na Gabriel Ng’osha
PENZI limekolea na kinachoonekana sasa kwa Ostaz Juma Namusoma ni kukazia penzi lake kwa mwanadada Blandina Chagula ‘Johari’ anayesumbua kwenye Bongo Muvi.

Habari zilizolifikia Amani kutoka kwa chanzo chetu zinasema kwamba Ostaz alifunga safari kwenda nchini Afrika Kusini kwa mapumziko mafupi lakini pia kumnunulia mpenzi wake huyo zawadi mbalimbali kwa lengo la kupalilia uchumba wao.

“Jamaa alikuwa Sauzi (Afika Kusini), aliondoka hapa tarehe 17 (Machi) na amerudi tarehe 21. Kamletea zawadi kibao lakini kubwa zaidi ni kamera kubwa, nzuri ya kisasa kwa ajili ya kerekodia filamu,” kilipasha chanzo hicho.

Amani lilifanikiwa kumpata Ostaz kwa njia ya simu, akafafanua: “Ni kweli nilikuwa Afrika Kusini. Kuhusu Johari, ni kweli si mke wangu? Nimemletea zawadi nyingi sana, achana na hiyo kamera unayosema.

“Lengo ni kuweka uchumba wangu  na yeye sawa. Nilitamani sana kusafiri naye lakini sikutaka kufanya hivyo ili kuweka usawa, mke wangu asione nimeegemea zaidi kwa mke mdogo.”

Alipoulizwa kwa nini amemuita Johari mkewe, haraka alisema: “Ndoa ipo karibu, nimeshaamua Johari awe mke wangu wa pili. Wadau wasubiri waone, uzuri ni kwamba dini yangu si kikwazo.”

hagula ‘Johari’ anayesumbua kwenye Bongo Muvi.

0 comments:

Post a Comment