Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, ishu
hiyo ilichukua nafasi maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako
Wema na Aunt wamepiga kambi kwa ajili ya filamu yao mpya ya Familia.
Ilidaiwa kuwa, Wema na Aunt ambao kwa
sasa wapo ‘kloz’ kiasi cha watu kuwa na maswali vipi kuhusu Kajala
Masanja, walipiga picha hizo wakidhamiria kuzifuta baada ya kujiona
lakini lililotokea si akili zao, picha hizo zikanaswa na paparazi wetu.
Juzi, Amani liliwatafuta kwa njia ya
simu wawili hao na kuwauliza nini kiliwatia nguvu hadi kupiga picha hizo
ambapo Wema anaonekana akibusu sehemu ya paji la uso la Aunt huku naye
akiwa amelegeza macho kusikilizia.
Wema: “Unajua huyu Aunt ni mtu ambaye
tumezoeana kupita kiasi, tunapomaliza kufanya kazi, tunaanza utani.
Halafu kwetu mbona mabusu ni ishu ya kawaida sana!”
Habari za ndani zinasema, baadhi ya
ndugu wa mume wa Aunt, Sunday Dimonte wamekuwa wakimtumia meseji ‘mista’
huyo kumweleza uchafu mbalimbali anaofanya mume wake licha ya kutotoa
tamko lolote.
Mbali na Dimonte, baadhi ya watu
waliozungumza na Amani walimtaka Nasibu Abdul ‘Diamond’ kukaa chini na
kufikiri upya kuhusu uamuzi wake wa kumuoa Wema. Wengi wanaamini si
sahihi kwake kwa vile haonekani ‘kutulia’ licha ya kwamba wote
‘hawajatulia’
0 comments:
Post a Comment