Mtafiti Mwanasayansi Irine Mremi, kutoka
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania
(NIMR) ambaye aliwasilisha ripoti hiyo kwa niaba ya watafiti wenzake wa
NIMR.
***
BAADHI ya wanawake kutoka katika Wilaya za Kinondoni, Tanga, Makete na Siha, wamekiri kufanya ngono kinyume na maumbile.
Hayo yalielezwa na Mtafiti Mwanasayansi
Irine Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu
nchini Tanzania (NIMR) wakati akiwasilisha utafiti uliofanywa na
watafiti wa NIMR juu ya ufanyaji Ngono kinyume na maumbile katika
kueneza maambukizi ya VVU/Ukimwi nchini na kuwasilishwa mbele ya
Wanahabari na Watafiti jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mremi amesema wanawake hao wamesema
chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni
kujipatia kipato zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda usichana wao na
baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.
“ Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na
wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika
jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu bar, wauguzi, makahaba na
akina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza
wakiwepo pia wanaume ambao wal;ihusishwa katika utafiti huo,” alisema
Mtafiri Irine.
Aidha alisema wakati wa utafiti huo
wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa wanafanya tendo la
kujamiiana kinyume na maumbile ambayo ni sawa na 26.5% huku 76.4% ya
waliohojiwa walidai kufanhamu njia hiyo ya kufanya mapenzi.
Wilayani Tanga ndio kumeonesha kukithiri
kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbe na wanaume
kuwafanyia wanawake kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako
bado kuna idadi ndogo.
Wanaume waliohojiwa katika utafiti huo
wamedai wao wanafanya kwa mtindo huo kwaajili ya kupata raha tu na imani
ya kuwa huko hakuna maambukizi ya VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia
mafuta ya aina mbalimbali ilhali matumizi ya mipira ikiwa ni hafifu
kwani wakitumia mipira wamedai kupunguza raha wanayo ipata.
Wanawake pia wamedai baadhi ya tamaduni
zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga msichana kuolewa na kukutwa
usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake na wazazi hivyo hulazimika
kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku suala la Mimba nalo likichukua
nafasi.
Watafiti hao wamesema ufanyaji huo wa
ngono kinyume na maumbile umekuwa ukisababisha michubuko kirahisi na
kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa kasi tofauti na kutumia njia ya
kawaida ya kujamiiana.
Aidha imedaiwa kuwa wanawake wengi
wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa
kujifungua kwa misuli yao ya kushindwa kuhimili kusukuma mtoto, jambo
ambalo limekuwa likileta tabu kwa wahudumu wa Afya hasa wakunga ambao ni
wachache mahospitalini kutumia muda mrefu kumhudumia mjazito mmoja huku
wengine wakiendelea kuteseka wodini wakati wa kujifungua.
Watafiti hao wameshauri elimu zaidi ya
kujikinga na maambukizi ya ukimwi na njia salama za kujamiiana
kufundishwa mashuleni ili kuondoa dhana ya kujamiiana kinyume na
maumbile kuwa haiambukizi virusi vya Ukimwi.
0 comments:
Post a Comment