Wednesday, February 11, 2015

Q Chief : "Mwambie TID aache kuvuta unga watu wote tushaacha sasa hivi..Tell him to do music not to talk about me"

 Kama ni mfatiliaji wa kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv, utakuwa umekutana na interview ya T.I.D  a.k.a Myama a.k.a Mzee Warioba akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho "Casto Dickson" lililohusu sababu kubwa ya kuvunjika kwa Top Band,ambapo kwa TID alisema Q Chilla alikuwa na tamaa.
*kama atadanganya mbele ya jamii kwamba nimempa chake na ye chake amekitumia tofauti kunichoresha sidhani kama ni mtu mzuri kwangu, ni mtu mbaya......
* Mwambie huyo Warioba kwamba Mugabe kakasirika kusikia una-provoke na kuongea vitu ambavyo havi-make sense kwake....
* aache kuvuta unga watu wote tushaacha sasahivi, afanye mambo ya msingi ana watoto ana baba ana mama aache kwanza ngada, arudi kwenye mziki kama mi nilivyorudi na For You, aache hizo habari ...
Q chief amefunguka maneno mazito sana baada ya kusikia kauli hiyo ya TID  
"sidhani kama hizo ni sababu, mi nadhani TID is alittle bit frustrated right now, because of what he is going through nadhani hilo linamfanya kidogo limchanganye na pale anapoulizwa maswali na kujibu. Katika kumbukumbu yangu mi ninachokumbuka ni kwamba muhindi alitoa kama milioni kumi hivi ya ile album, alivyotoa ile ilikuwa ni advance bado tunamdai hela ingine  mi nilikuwa nimesafiri nimeenda Mombasa, kwahiyo my only mistake nikumwambia TID kwamba nende kachukue ile hela kwa muhindi nikiwa na imani ni hela ndogo hawezi kuitolea macho....
.
Unajua hela ni hela, hela ni ibilisi alivyoishika mkononi, alikuwa kijana alikuwa  na mambo mengi, akaingia tamaa, kuingia tamaa akaniambia bwana kuna milioni tatu imetoka inabidi nikupe nini, halafu kwanza na mi pia nimechukua tatu halafu kuna nne nyingine itatoka, kwahiyo aka-compile zile mbili zangu mbili zake zikawa nne  kwa hiyo ana seven milion, mi narudi baada ya wiki moja namwambia bana sasa inabidi tupande ndege twende Dubai tukachukue vyombo, mi na wewe tukachague, baadae nikapiga hesabu kiubinaadam na kiungwana nikaona aah tukipanda ndege watu wawili cost itakuwa nyingi, kwanini wewe usiende tayari una experience na Band, basi tumepanga vizuri, namkuta asubuhi anakula bata, mi natoka maisha nasema huyu si Myama huyu, anatakiwa awe kwenye ndege saa hii, sa mbona yuko hapa? mtu wa pembeni girlfriend wake akanitonya akaniambia sikiliza TID akiona hela anakuwa kama jini anabadilika na ubinaadam pia unakwisha..........
Sasa TID kumbe ile hela kaila kaifanyia mambo mengine kaongezea kanunua gari, mi nilivyorudi nikamfat amama ake na kaka zake, nikawaambia bwana ikija mara ya pili ntakuja na defender za kutosha halafu ntamuharibia huyu jamaa umeon abwana. sasa wakaja wakanitisha bwana unajua TID sijui mtu wa kinondoni, nikawaamba mi staki kuju anaishi wapi kwasababu mi mwenye mtoto wa jua, Sun of the Sun no mother no father, nimezaliwa na jua, sa ukiniambia kazaliwa oooh sijui wapi sijui wapi me i really dont wanna know that, me i want my money back, ndio maana kesho nakuja na polisi.....nilivyofika na polisi wakaomba negotiation (maelewano) pia hakutoa hiyo hela yote aliyokusudiwa kuitoa milioni tatu iliyobaki, jamsingi alichokifanya kajipiga piga kaja akatoa milioni moja na nusu.........
Infact i dont like the guy kwasababu he is a bit frustrated he needs to sit down and settle his things, thats how he can sit down na kuanza maisha mapya, nilihisi tumeshayamaliza haya mambo, lakini kama atadanganya mbele ya jamii kwamba nimempa chake na ye chake amekitumia tofauti kunichoresha sidhani kama ni mtu mzuri kwangu, ni mtu mbaya......
Qchief aliendelea kutiririka baada ya swali kuhusu kama kutakuwa na uwezekano wa baadae kurejea top band 
no no no no am another new brand yaani, ni brand kubwa kuliko ye anavyofikiria sidhani kama mimi napaswa kurudi Top Band, nadhani yeye anaendelea, afanye kitu Top Band irudi pale, kwasababu siisikii siioni, kwahiyo unaponiambia nirudi pia ur making a mistake, Qchief amerudi kwaajili ya kufanya kazi zake na wasanii wanao focus na future yao, sio wasanii ambao wako tayari ku-back bite kuhusu mtu flani kwasababu ya wao kupata kiki......
Mwambie huyo Warioba kwamba Mugabe kakasirika kusikia una-provoke na kuongea vitu ambavyo havi-make sense kwake, tell him to do music, better music, not to talk about me cause me i dont talk about him anymore, na aache kuvuta unga watu wote tushaacha sasahivi, afanye mambo ya msingi ana watoto ana baba ana mama aache kwanza ngada, arudi kwenye mziki kam ami nilivyorudi na For You, aache hizo habari. Aachane kabisa na mambo ya unga, arudi, akiri awe mwanaadamu kama wanaadamu wengine, unakuwaje mnyama, unakuwaje mnyama wakati we binaadamu. mwambie sasa mzee mugabe kashafanya Press Conference nyingi kuliko Mzee Warioba kacheza na International Affairs amulizie Mugabe nani duniani atapata majibu

0 comments:

Post a Comment