likua
jumatatu, tarehe 10 mwezi wa 6 mwaka 2013,niko kwenye msiba wa kaka
angu(RIP BRO).. Ilikua kama sa 2 hivi usiku niko kwenye kikao tukijadili
na kupanga taratibu za mazishi,kuhifadhi mpendwa wetu.
Nikiwa
kikaoni nikasikia mtetemo kwenye sim yangu ikiashiria ujumbe mfupi
umeingia,sikua na haraka ya kuusoma,nikijua baada ya kikao ntausoma,ndio
ntakua na muda mzuri wa kusoma ujumbe huo,hata hivyo mimi ndie nilikua
katibu wa kikao,nikakipa kikao uzito zaidi.
Ilipofika
sa 4 kama na nusu hivi kikao kimeisha, nikasikia mlio wa sim,ilikua ni
sim yangu ikiita,nikaitoa mfukoni kuipokea,kusoma jina ni la kipenzi cha
moyo wangu,nikatabasam kwa mbali nikijua mpenzi wangu kanipigia kujua
naendeleaje,ile napokea tu sim ikakata.
Nikajua
mamaa kaishiwa pesa,nikaenda hewani,simu ikaita kidogo kisha
nikasikia"simu ya mteja uliepiga inatumika" ikiashiria sim
imekatwa,nikakata sim,mara kidogo nikapokea ujumbe kutoka mpenzi wangu
"nilitaka
kujua kama meseji umeipata,sitaki mapenzi na wewe,futa namba yangu"
nikashtuka kidogo,nikajua ni utani,kisha nikataka kujua ni ujumbe gani
huo
Nikaenda
inbox nikakuta ujumbe uliokua umetumwa haujasomwa ni wake akinijulisha
mimi na yeye basi. Nikampigia sim hapokei,nikatuma ujumbe hakujibu.
Msiba wa ndugu yangu ukawa mchungu zaidi
Siku
zikaenda hivyo nikiwa siamini kilichotokea,bila ugomvi,bila sababu ya
msingi nikawa nimeachwa. Nikatumia kila mbinu kumbembeleza na
kumshawishi,kupitia kwa ndugu zake,marafiki zangu na ndugu zangu
akagoma.
Ratiba
zetu ilikua mwezi wa kumi mwaka jana nikajitambulishe rasmi,mwezi wa
pili mwaka huu tufunge ndoa . Mipango hiyo ikawa imekufa. Niliyumba sana
baada ya hilo tukio,nimejikaza nikasimama kiume ila kwa maumivu makali
sana.
Kituko
cha mwaka ni kua binti huyo kamwambia rafiki yangu kua bado ananipenda
na anatamani turudiane, hadi naandika ujumbe huu huyo binti toka juzi
anapiga sim(sijapokea simu yake hata moja) na kutuma ujumbe akiniomba
nimsamehe
Wadau,nimrudie
kisha nimtende kama alivyonifanya au nimuache aendelee na maisha
yake(sina hisia nae tena na wala simpendi,,namchukia sana,natamani
kisasi juu yake),ebu nishaurini wandugu.
0 comments:
Post a Comment